Rais Tinubu wa Nigeria anasema mauaji ya wanajeshi katika Jimbo la Abia, kusini-mashariki mwa Nigeria, na kundi lililopigwa marufuku siku ya Alhamisi yalikuwa ”babaric” na ”mabaya” na jeshi litachukua hatua ”maamuzi” kujibu.
Wanajeshi watano walishambuliwa na watu wenye silaha waliojifunika nyuso zao wakitekeleza amri ya kukaa nyumbani iliyotangazwa na kundi lililoharamishwa, Indigenous People of Biafra (IPOB), kuadhimisha Siku ya Biafra kote kusini mashariki mwa nchi.
”Nimepokea habari nyingine ya kukatisha tamaa kuhusu kuuawa kwa wanajeshi watano na watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa shirika lililopigwa marufuku la kigaidi, IPOB. Vitendo hivi vya kinyama na viovu visivyostahili ni vya kulaaniwa na havipaswi kamwe kusamehewa au kuvumiliwa katika nchi yetu.” Tinubu alisema katika taarifa yake iliyochapishwa kwenye mtandao wa X.
Siku ya Biafra hutangazwa Mei 30 kila mwaka na IPOB kuwakumbuka watu waliofariki kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka mitatu, vilivyozuka Mei 30, 1967, baada ya maafisa wa jeshi la Igbo kutangaza jimbo huru la Biafra.