Wastani wa umri wa watu wanaovuta sigara kwa mara ya kwanza kumetajwa kuwa miaka 7, hii ni kiulingana na takwimu za Shirika la Afya Duniani nchini Tunisia.
Takriban 20% ya vifo katika taifa hilo la Afrika Kaskazini vinahusishwa na uvutaji sigara na athari zake mbaya.
Dk Olfa Saidi, afisa wa WHO anayehusika na magonjwa yasiyo ya kuambukiza na afya ya akili nchini Tunisia, alisema kuna ongezeko la watumiaji wa tumbaku miongoni mwa vijana.
Alisema kuwa kupatikana kwa sigara za kielektroniki na tumbaku iliyopamba moto kumewashawishi vijana wengi zaidi kuvuta sigara.