Katika kuendeleza Kukuza kiwango cha elimu nchi Halmashauri ya Mji wa Babati Mkoani Manyara imetoa Pongezi na vikombe vya heshima kwa shule zilizofanya vizuri katika matokeo ya wanafunzi wa darasa la nne na darsa la Saba.
Hayo yamefanyika katika Mji wa Babati Mkoani Manyara ambapo shule ya Deira English Medium School imeongoza kwa kufanya vizuri katika Mji wa Babati ambapo Mkuu wa Shule hiyo amesema “Huu ni Ushindi baada ya matokeo ya darada la saba na darasa la nne 2023,shule yetu imefanya vizuri kwa mitihani ya Taifa tumekabidhiwa makombe mawili Kwa kuwa shule Bora, Mafanikio haya ni juhudi za waalimu wanafunzi pamoja na wazazi wenyewe pamoja na Motisha wanayopata waalimu na wanafunzi haya ndio yametupa muunganiko na kupata Ushindi huu” Mkuu wa Shule Paulo Dallo.
Nao wazazi walioshiriki katika zoezi hilo Wamesema Matarajio Yao kama wazazi nikuona watoto wao wakifanya vizuri nakupongeza juhudi zilizofanywa na shule hiyo ya Deira Kwa kuwa msingi wa Maisha ya mtoto ni elimu bora pamoja na Malezi Bora ambayo yanapatikana shuleni hapo.
Aidha Wamesema katika suala la Malezi kwa watoto ni jukumu la watu wote na sio waalimu Pekee,hivyo kuwaomba wazazi kuendelea kusimamia Maadili ya watoto wao bila kuwaachia waalimu pekee pamoja na Serikali.
Naa wanafunzi akiwemo Faridi Kimweri wamesema wanajivunia kuwepo katika shule hiyo yenye Mafanikio ambapo Kuna waalimu wenye weledi katika ufundishaji pamoja na usafiri wa uhakika kwa wanafunzi jambo linalowafanya kufanya vizuri katika taaluma.