Korea Kusini inapanga kusitisha makubaliano ya kijeshi yaliyotiwa saini na Korea Kaskazini mwaka 2018 kwa lengo la kupunguza mvutano, ofisi ya rais ilisema Jumatatu, baada ya Seoul kuonya kuhusu jibu kali kwa puto zilizozinduliwa na Pyongyang kubeba taka kuelekea Kusini.
Korea Kaskazini imerusha mamia ya puto zilizobebwa na upepo kuvuka mpaka na kutupa takataka kote Korea Kusini, ambayo iliita kuwa ni uchochezi na kukataa madai ya Pyongyang kwamba ilifanywa ili kumsumbua jirani yake.
Baraza la Usalama la Kitaifa lilisema litaibua mpango wa kusitisha makubaliano yote ya kijeshi ili kuidhinishwa na baraza la mawaziri katika mkutano wa Jumanne.
Kusitishwa kwa makubaliano hayo kutafungua njia kwa Kusini kuendesha mafunzo karibu na mpaka wa kijeshi na kuchukua “hatua za kutosha na za haraka” kujibu chokochoko za Korea Kaskazini, Baraza lilisema katika taarifa yake.
Haikufafanua hatua hizo zinaweza kuwa nini.