Mwenyekiti wa kikundi cha wanawake cha Generation Queens mkoani Pwani, Betty Msimbe amewaasa wanawake kuendelea kujituma ili kujikomboa kimaisha na kuondokana na zama za utegemezi.
Akitoa rai baada ya kutoa tuzo ya KAZI IENDELEEE AWARDS kwa makundi mbalimbali ikiwemo wajasiriamali , kwenye sherehe ya Umoja wa kikundi hicho , alieleza wanawake kwasasa sio muda wa kupoa ,ni lazima kujishughulisha kuweza kujiimarisha kiuchumi na kimaendeleo.
Vilevile alieleza, katika utoaji wa tuzo ni mara ya tatu sasa na itakuwa ni jambo Endelevu.
Tuzo hizo zimetolewa kwa kuunga mkono juhudi za mikono ya wanawake na kuwapa moyo kuendelea kujituma ,sanjari na kuunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais dkt.Samia Suluhu Hassan ambae kwa asilimia 100 amekuwa ni mfano kwetu akinamama kuchapa kazi kwa bidii” alifafanua Msimbe.
Pia alisema ,walianzisha kampeni ya KOMBOA WATOTO WENYE ULEMAVU ambapo lengo lao kupata baiskeli 100 lakini hadi sasa wameshatoa 26.
Mgeni rasmi na Mwenyekiti wa Jukwaa la Uwezeshaji Kiuchumi Wanawake Mkoa wa Pwani ,Mariam Ulega aliwataka wanawake kuiga kwa vitendo yale mazuri yanayofanywa na Rais Dkt Samia Suluhu katika kuwekeza kwa wanawake na kusimama nao kidete ili kuwa chachu ya maendeleo ya Tanzania.
Pia Mariam liipongeza Kikundi hicho Mwanamke Sahihi Fete kwa jitihada za kumuinua mwanamke wa Pwani.
‘Kwa kipekee ,Mariam Ulega alishukuru kupata Tuzo ya heshima kutokana na jitihada zake za kusaidia jamii ‘.
“Mimi ni yatima ,Baba yangu alifariki nikiwa na miaka mitano,mama yangu amefariki nikiwa na miaka 6 ,nilikuwa nikisaidiwa na jamii ya mtaani kwetu,hawakunitupa ,walinilea usiku na mchana.”
“Kutokana na hilo huwa na Mimi nakumbuka nilipotoka nachokipata Leo narudisha Kwa wengine wenye mahitaji “alifafanua Mariam Ulega.