Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba amesema hadi kufikia Aprili 2024, Bodi ya Michezo ya Kubahatisha imetoa jumla ya leseni 9,805, sawa na ufanisi wa asilimia 82 ya lengo la mwaka ambapo kati ya kiasi hicho, leseni 6,261 zimehuishwa na 3,544 ni leseni mpya.
Akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Mwaka 2024/2025, Bungeni Jijini Dodoma leo June 04,2024, Mwigulu amesema “Kwa mwaka 2023/24, Bodi ya Michezo ya Kubahatisha ilipanga kutoa leseni 11,880 kwa waendesha michezo ya kubahatisha, ambapo 2,273 ni leseni mpya na leseni 9,607 ni za
32 kuhuisha, kufanya ukaguzi kwa waendesha michezo ya kubahatisha 101 na kusimamia mchakato wa uendeshaji wa Bahati Nasibu ya Taifa.
“Aidha, Bodi imekagua jumla ya Waendeshaji 87 wa michezo ya kubahatisha, sawa na asilimia 86 ya lengo la mwaka, vilevile Bodi imeteua kampuni ya kuendesha Bahati Nasibu ya Taifa na tayari imesaini mkataba wa uendeshaji kwa mujibu wa sheria ya michezo ya kubahatisha”