Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba amesema hadi kufikia Aprili 2024, Wizara hiyo imefanikiwa kukusanya jumla ya shilingi trilioni 32.49, sawa na ufanisi wa asilimia 82 ya lengo la mwaka ambapo kati ya kiasi hicho, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekusanya jumla ya shilingi trilioni 21.31, Idara ya Fedha za Nje shilingi trilioni 4.92, Idara ya Usimamizi wa Deni la Serikali shilingi trilioni 6.18 na maduhuli kupitia Fungu 23 shilingi bilioni 79.23 na Fungu 50 shilingi milioni 950.
Akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Mwaka 2024/2025, Bungeni Jijini Dodoma leo June 04,2024, Mwigulu amesema “Wizara ya Fedha ilikadiriwa kukusanya shilingi trilioni 39.79, kati ya makadirio yote ya Serikali ya kukusanya jumla ya shilingi trilioni 44. 39 kwa mwaka 2023/24”
“Kati ya kiasi hicho, Fungu 21 lilitarajiwa kutafuta na kukusanya jumla ya shilingi trilioni 39.74 ambapo Mamlaka ya Mapato Tanzania ilikadiriwa kukusanya shilingi trilioni 26.73, Idara ya Fedha za Nje shilingi trilioni 5.47 na Idara ya Usimamizi wa Deni la Serikali shilingi trilioni 7.54, Fungu 23 lilikadiriwa kukusanya shilingi bilioni 60 na Fungu 50 shilingi milioni 300”