Ikiwa Club ya Yanga leo imepewa Tsh milioni 537.5 na Mdhani wao wa Mkuu SportPesa kama sehemu ya zawadi (bonus) ya kufanya vizuri katika msimu wa 2023/2024.
Hundi hiyo imepokelewa na Rais wa Yanga Hersi Said kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa SportPesa Abbas Tarimba, hiyo ni kama motisha kwa Yanga ya kuhakikisha wanaendelea kufanya vizuri.
Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa Sport Pesa Mhe.Abbas Tarimba amempongeza Ghalib Said Mohamed (GSM) kwa mchango wake kwenye klabu ya Yanga SC…
“Nimpongeze sana Rais wa Young Africans SC Injinia Hersi Said kwa jitihada zake kwa Klabu hii. Sisi kama Kampuni ya @tzsportpesa vile vile tunampongeza Mdhamini na Mfadhili wa Young Africans SC Ghalib Said Mohamed (GSM) kwa mchango wake mkubwa kwa Klabu hii. Bila shaka amefanya kazi kubwa, tunapenda salamu zetu zimfikie” Mkurugenzi Mtendaji wa @tzsportpesa Mhe. Abbas Tarimba