Serikali kupitia Wizara ya Kilimo imetenga kiasi cha shilingi bilioni 7.5 kwaajili ya awamu ya kwanza ya ujenzi wa viwanja vya maonyesho ya Nanenane jijini Dodoma ambayo kwa mwaka 2024 kitaifa yanafanyika mkoani Dodoma na mgeni rasmi wa ufunguzi anatarajiwa kuwa makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango.
Taarifa hiyo imetolewa na Waziri wa Kilimo Hussein Bashe alipokuwa akizungumza na wanahabari jijini Dodoma ambapo amesema awamu hiyo ya kwanza ya ujenzi itaanza na ujenzi wa Fensi na Barabara za ndani ya uwanja.
akizungumzia maonesho ya Nanenane waziri Bashe amesema maonesho hayo yanatarajiwa kuanza tarehe 01 Agosti, 2024 “bahati nzuri mpaka sasa tumeshapata baadhi ya nchi Jirani ambazo zimeonesha nia ya kuja kushiriki kwahiyo taswira ya nanenane ya mwaka huu itakuwa na washiriki baadhi kutoka nje ya nchi ambayo ni makampuni mbalimbali yanayonunua bidhaa za Tanzania ama yanayouza huduma katika soko la Tanzania” Waziri wa Kilimi Hussein Bashe