Wanasayansi wameonya Watu wasinywe pombe kabla ya kulala kwenye ndege wakisema kipindi ambacho ndege ipo futi 8,000 angani, viwango vya hewa ya oxygen pamoja na presha ya hewa huwa vipo chini kuliko hali ya kawaida Duniani na kwamba yote hayo yakichanganywa na vilevi pamoja na usingizi kuna uwezekano mkubwa zaidi kwamba viwango vya oxygen katika damu ya binadamu vitapungua ikapelekea Mtu kupata magonjwa ya moyo pamoja na changamoto kwenye mapafu kwa mujibu wa utafiti uliochapishwa katika jarida la Thorax.
Watafiti hao walitengeneza mazingira yanayofanana na mandhari yaliyopo ndani ya ndege kwa zaidi ya siku mbili ambapo Watu wazima 48 wenye afya nzuri walilala kwa saa nne wakati mmoja wakiwa hawajachukua kileo chochote huku wakati mwengine wakinywa glasi mbili za wine au bia na kulingana na ilipofika usiku kiwango cha oxygen kilionekana kupungua Watu hao wakiwa wamekunywa pombe kisha kulala huku mapigo ya moyo pia yakiongezeka na pia uwezo wa kuimarisha kumbukumbu kwenye ubongo pia ulipungua.
Watafiti pia wamesema unywaji wa kahawa au energy drinks na kukaa muda mrefu bila maji sio sahihi kutokana na mazingira ya angani kuwa makavu huku pia vyakula vinavyotolewa kwenye viwanja vya ndege na ndani ya ndege vinaweza kuwa na chumvi na mafuta, kwahiyo Watu wanatakiwa wanywe maji mengi.