Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Tanzania (HESLB) imefungua dirisha la kupokea maombi ya Mkopo kwa mwaka 2024/ 2025 kwa wanafunzi wa ngazi mbalimbali ya vyuo vikuu ambapo kiasi cha Shilingi Bilioni 787 kimetengwa kwa wanafunzi 224,056.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo Dkt. Bill Kiwia amesema uombaji wa Mikopo unaanza June 6, 2024 hadi August 31,2024 na hakutakuwa na dirisha la pili la maombi ya mkopo huo hovyo kuwahimiza wanafunzi kuanza mara moja kuomba mkopo
“Tumetoa muda wa miezi 3 kwa wanafunzi kuomba mkopo, mudahuu no mrefu zaidi na tunaamini unatosha kwa wanafunzi kukamilisha zoezi hilo ndani ya muda na baada ya hapo hatutakuwa na muda mwingine ” amesema Dkt Bill Kiwia
Mbali na hilo pia amesema “Kama mtakavyokumbuka, katika mwaka wa fedha 2024/2025, Serikali imetenga TZS 787 bilioni kwa ajili ya mikopo na ruzuku kwa jumla ya wanafunzi 250,000. Idadi hi ya wanafunzi imeongezeka kutoka wanafunzi 224,056 mwaka 2023/2024. Hivyo, mwaka ujao wa masomo kutakuwa na ongezeko la jumla ya wanafunzi takribani 25,944,”
“Wito wetu kwa wanafunzi wanaoomba mkopo ni kuhakikisha wanatimiza wajibu wao kwa kusoma miongozo iliyotolewa na kuizingatia wakati wa kuomba mkopo,”
Tunafahamu kuwa katika kipindi cha uombaji mikopo, wanafunzi huwa na maswali au maoni. Hivyo, katika kipindi hiki cha kuomba mkopo, Kituo cha Huduma ya Simu (HESLB Call Centre) kipo wazi kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 11 jioni,”