Naibu Gavana wa benki kuu aneshughulikia masuala ya uchumi na sera ya fedha Dkt Yamungu kayandabila amekitaka chuo cha benki kuu kuwa karibu na wananchi ili kusaidia wananchi kuendana na kasi ya mabadiliko katika sekta ya fedha yanayoletwa na maendeleo ya teknolojia katika sekta hiyo
Ameyasema hayo jijini Dar es salaam wakati akikabidhi vyeti 86 vya ithibati ya weledi kwa wataalamu wa utoaji wa elimu ya fedha kwa umma waliopatiwa mafunzo kutoka chuo cha benki kuu
Akizungumzia mafunzo hayo naibu gavana amesema , kupitia mafunzo hayo benki kuu inataraji kuona umma ukielimika vya kutosha juu ya viwango vya riba vinavyotolewa na taasisi za fedha hatua itakayosaidia kupunguza changamoto ya uwepo wa mikopo umiza ambayo mingi imekuwa ikisababishwa na wanachi kutoelewa mchanganuo wa kiwango cha riba anachotakiwa kurejesha na kwa muda gani
Miongoni mwa mafunzo yaliyotolewa na chuo hicho kwa muda wa wiki mbili ni pamoja na ujuzi wa hesabu za fedha , ulinzi binafsi wa fedha, usimamizi wa fedha na ikolojia ya fedha