Rais wa Yanga, Eng. Hersi Said amesema Mdhamini na Mfadhili wa Yanga, GSM yupo tayari kutekeleza mradi wa ujenzi wa uwanja na kusema GSM hajawahi kutoa ahadi hewa, hivyo Hersi amewaahidi Wanachama na Mashabiki kuwa mchakato upo tayari kuanza kwa kuzingatia mradi wa Mto Msimbazi.
Akiongea leo June 09,2024 kwenye Mkutano Mkuu wa Yanga Jijini Dar es salaam, Hersi amesema “Naawahidi Mashabiki na Wanachama tutafanya usajili mkubwa sana msimu ujao, msimu ujao tutafanya mambo makubwa kuanzia ndani na nje ya mipaka ya Tanzania, tutafanya Pre season nzuri, tumeshapata mialiko maeneo mbalimbali ikiwemo Afrika Kusini, Kaizer Chiefs wametoa mwaliko na Mh. Raila Odinga ametuomba tuungane nao kwenye uzinduzi wa uwanja wao huko Kisumu pamoja na Nchi moja ya ulaya”
“Leo tupo na Mheshimiwa Mchengerwa, na tayari amepokea maombi yetu kuhusu mchakato wetu wa ujenzi wa uwanja wetu hapa Jangwani, jambo la kheri ni kuwa amejumuika nasi moja kwa moja akitokea Tabora, mradi wetu huu wa ujenzi wa uwanja tayari upo ofisini kwake na analifanyia kazi”