Benki ya NCBA Tanzania inajivunia kutangaza ushirikiano wake na Rotary Club ya Bahari Beach Dar es Salaam katika mashindano ya 13 ya kila mwaka ya golf kwa ajili ya kuchangia shughuli za kijamii, yaliyofanyika tarehe 8 Juni, 2024, katika Klabu ya Golf ya Gymkhana Dar es Salaam.
Mashindano hayo, yaliwaleta pamoja wacheza golf na wadhamini kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania, yakilenga kukusanya fedha kwa ajili ya miradi ya kijamii. Tukio la mwaka huu lilijikita katika kusaidia swala zima la STEM jijini Dar es Salaam na Zanzibar, chini ya kaulimbiu “Elimu Bora na ya kisasa kwa Kilimo cha Kesho.”
Bw. Claver Serumaga, mkurugenzi mtendaji wa NCBA Tanzania akicheza golfu, alionyesha furaha yake juu ya ushirikiano huu akisema “Benki ya NCBA imejikita katika kusaidia elimu na miradi ya maendeleo ya kijamii. Tunajivunia kushirikiana na Rotary Club ya Bahari Beach Dar es Salaam katika juhudi hizi za zenye tija kwa nchi yetu.”
Mbali na kudhamini Mashindano ya Golf ya Rotary, Benki ya NCBA inajiandaa kuandaa Mashindano ya Golf ya NCBA Bank maarufu kama NCBA Golf Series huko Arusha, Tanzania, tarehe 29 Juni, 2024. Tukio hili, linaonyesha dhamira ya benki hii katika kuendeleza michezo hususani mchezo wa golf nchini Tanzania pamoja na juhudi zao kwenye kuikwamua jamii katika nyanja mbalimbali.