Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Jingu, Juni 7, 2024, akiwa ameambatana na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu, ameongoza Mkutano wa Afya wa DPG 2024 unaolenga kuendeleza ushirikiano baina na Serikali na Wadau wa Maendeleo na Afya.
Mkutano huo ambao umefanyika katika ukumbi wa ofisi ndogo za Wizara jijini, Dar Es Salaam, umeshirikisha wadau wa Maendeleo na Afya kutoka Troika, HSRS, Irish Aid, WHO na Benki ya Dunia na Sekretarieti ya Wizara ya Afya.
Ajenda kadha wa kadha zilipata kujadiliwa ikiwemo kuzidisha mashirikiano baina ya pande hizo mbili katika njia mbalimbali zitakazo saidia kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya Afya nchini ikiwemo suala la ugharamiaji na gharama za matibabu ili kuimarisha ubora wa huduma.
Katika mkutano huo Dkt.Jingu amewashukuru wadau hao kwa namna wanavyoendelea kushirikiana na Wizara ya Afya katika kuendeleza afua zake, pia amemshukuru Mwenyekiti wa Troika anaemaliza muda wake Mariam Ally, Mwenyekiti Matthew Cogan na kumkaribisha Mwenyekiti mpya wa Troika Mustapha Abdallah.