Pep Guardiola anatumai Bernardo Silva atasalia Man City, kwa mujibu wa The Sun.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 alijiunga na City kutoka Monaco mwaka 2017 na amekuwa akihusishwa na kuhamia Barcelona.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno alitia saini nyongeza ya kandarasi mwaka jana ili kumaliza uvumi kuhusu hatma yake – lakini mkataba huo una kipengele cha kuachiliwa kwa pauni milioni 50.
Akizungumza katika mashindano ya gofu ya Legends Trophy, Guardiola alisema: “Barca haijawahi kupiga simu [kuhusu Bernardo]. Kumekuwa na mazungumzo mengi kwa miaka lakini hakuna aliyetupigia simu.
“Natumai atasalia, ni mchezaji wa msingi kwetu, jiti la mchezaji, kama mtu. Ukitaka mchezaji lazima umite, na haijafanyika.”