Newcastle United wamekubali mkataba wa miaka mitano na beki wa Bournemouth Lloyd Kelly.
Kelly anatarajiwa kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu na kusaini mkataba huo, ambao unajumuisha chaguo la kurefusha kwa miezi 12, wiki hii.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 atakuwa mchezaji huru wakati muda wake wa kutumikia klabu Bournemouth utakapokamilika Juni 30, huku klabu hiyo ya kusini mwa pwani ikithibitisha kuondoka kwake baada ya kumalizika kwa msimu wa 2023-24.
Newcastle walikuwa na nia ya kukamilisha dili la kumnunua Kelly baada ya kukosa mlengwa mwingine wa safu ya ulinzi Tosin Adarabioyo, ambaye amejiunga na Chelsea kwa uhamisho huru kutoka Fulham.
Kulikuwa na nia ya Ulaya kwa Kelly lakini Muingereza huyo badala yake ataungana na Eddie Howe, ambaye alimpeleka Bournemouth kutoka Bristol City mnamo 2019.
Uwezo wa Kelly kucheza katika nafasi ya beki wa kushoto na beki wa kati ulivutia Newcastle, ambao walitaka yeye na Tosin kutokana na Sven Botman na Jamaal Lascelles kuwa nje na majeraha ya anterior cruciate ligament (ACL). Kelly anaondoka Bournemouth akiwa ameichezea klabu hiyo mechi 141 ndani ya miaka mitano.