Wasanii kumi tofauti kutoka katika taaluma mbalimbali za ubunifu wanatarajiwa kuwezeshwa kwa kupewa mafunzo, vifaa na ujuzi wa kutumia nguvu yao ya sanaa kwa ajili ya mabadiliko ya kijamii.
Fursa hiyo inatajwa kuwa muhimu kwa Wasanii kujihusisha kwa kina na masuala muhimu ya kijamii, kutumia vipaji na talanta zao za ubunifu ili kuleta matokeo yenye maana na kuhamasisha mabadiliko chanya kwenye Jamii.
Nafasi Art Space, kwa kushirikiana na ForumCiv, imezindua ushirika huo wa sanaa Nchini Tanzania hatua ambayo inaashiria mpango wa mwanzo kabisa wa mafunzo ndani ya mandhari ya kisanii nchini.
Msimamizi Mkuu wa Ukanda wa Afrika Mashariki Jackson Kimari amesema kuwa lMafunzo rasmi yanatarajiwa kuanza Juni 10 hadi Septemba 30, 2024, lengo kuu ni kufanya mabadiliko kwa Jamii”