Maandishi mapya yaliyofasiriwa yanayoturudisha nyuma katika kipindi cha miaka zaidi ya 1,600 iliyopita yamegunduliwa, Maandishi hayo yanazungumzia kile kinachoitwa maisha ya awali kabisa ya Yesu Kristo katika enzi za utoto wake.
Maandishi hayo yameandikwa katika mafunuo yanayokadiriwa kuwa ya karne ya 5 au 6 ambapo yamehifadhiwa maktaba huko Humbarg, Ujerumani kwa miongo kadhaa na yamejulikana kwa muda mrefu kuwa yenye umuhimu.
Hata hivyo wataalamu wawili wamefanikiwa kutafsiri maandishi hayo wakisema kuwa ni kopi za mwanzo kabisa zinazoishi za kitabu cha utoto cha injili ya Thomas, Lajos Berkes mwalimu wa thiolojia amethibitisha.
Berkes amesema kuwa mwanzoni mwa utafiti wao kufasiri maandishi hayo walidhani kuwa yatakua ni barua ya siri au orodha ya mahitaji ya vitu lakini walipogundua neno Yesu katika maandishi hayo ndipo walipoanza kupambana kuyatafsiri.
Kipande cha mfunjo wa maandishi hayo kina mistari 13 yenye herufi za kigiriki na inatoka Misri ya kale ambayo ilikua jamii ya kikristo kwa wakati huo, Maandishi hayo yanaelezea mwanzo wa “Uamsho wa Shomoro” ambayo inazungumzia utoto wa Yesu.
Stori hiyo inaelezea kuhusu Yesu alivyougeuza udongo wa mfinyanzi kuwa ndege hai wanaoruka, Kwa mujibu wa stori hiyo inaeleza kuwa Yesu alikua akicheza na watoto wengine ndipo alipofanya ajabu hilo la kugeuza maumbo ya mfinyanzi kuwa kiumbe hai.
Inaelezwa kuwa huo ulikua muujiza wa pili kuufanya Yesu kama ilivyoelezwa katika kitabu cha “The Infancy Gospel Of Thomas” kinachoelezea historia ya kale kuhusu Yesu na maajabu aliyofanya katika utoto wake.
Gazeti moja (Time) liliripoti kwamba vitabu vingi zaidi vimeandikwa kumhusu Yesu kuliko mtu mwingine yeyote katika historia. Vingi kati ya vitabu hivyo hujibu swali, Yesu ni nani? Yaelekea kwamba kumekuwa na ubishi mkubwa zaidi kuhusu suala hilo kuliko kuhusu habari nyingine yoyote katika historia ya wanadamu.