Shirika rasmi la habari nchini Tunisia liliripoti Jumanne kwamba raia 23 wa Tunisia wamefariki walipokuwa wakitekeleza ibada ya Hija katika Ufalme wa Saudi Arabia.
Shirika hilo lilinukuu chanzo kutoka kwa Ubalozi mdogo wa Tunisia mjini Jeddah. Majina ya watu hao, wanaume na wanawake, yalichapishwa kwenye ukurasa wa Facebook wa ubalozi huo. Jamaa walitakiwa kuwasiliana na mamlaka.
Imeripotiwa na Guardian kwamba “angalau 550” mahujaji wa mataifa mbalimbali wamekufa kutokana na joto la juu kupita kiasi nchini Saudi Arabia wakati wa Hija, ambayo inakaribia mwisho. Mamlaka ya Saudia ilisema kuwa mahujaji 2,000 wanatibiwa magonjwa yanayohusiana na joto.