Wafugaji katika tarafa ya Idodi Mkoani Iringa wametakiwa kukubaliana na wakulima mara baada ya mavuno ili kupata malisho kwa wajili ya mifugo yao.
Kwa mujibu wa Afisa Tarafa wa Idodi Mapsa Makala alisema kutokana na changamoto ya moto katika maeno mbalimbali ya tarafa ya idodi yanatokana na wafugaji wenyewe kwani wamekuwa wakiwalazimisha wakulima kuvuna mapema mazao yao ili wapate malisho ya mifugo.
Alisema wafugaji wanapaswa kukaa mza moja na wakulima na kuingia makubaliano ya kuuziana mabaki hayo ya mazao ikiwemo mabua ya mahindi ili kuondoa migogoro baina yao
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Idodi Mh. Julius Modestus Mbuta alisema kutokana na kutokuwepo kwa makubaliano baina ya wakulima na wafugaji imekuwa ikipelekea migogoro na hivyo wakulima kuchoma mashamba yao kutokana na wafugaji kutumia nguvu
Hiyo imtokana na baadhi ya wafugaji kulalamikia changamoto ya moto hali inayosababisha mifugo yao kukosa malisho
“wafugaji tumekuwa kama watoto wasio na baba au mama tuna pori kubwa kwaa ajili ya malisho wakulijma wa kijiji hiki kwa sasa kuanzia miaka 2 kwenye eneo ambalo limetengwa ng’ombe hawawezi kuchunga kwa muda wa kifuku kwa maana mashamba yamejaa kwa hiyo mimi nafikiri kero yetu sawa tulipewa lakini kwa sasa ndipo ilipo mashamba kulikuwa na mkutano kwa ajili ya watu wanaolima maeneo hayo kwa hiyo kero ndivyo ilivyo“ Alisema mmoja wa wafugaji.
Katika hatua nyingine jamii ya wafugaji waliaswa kuwapeleka watoto shule ili kupata watetezi na kuwatatulia baadhi ya changamoto zilizokuwa zikiwakabili .