Utekelezaji wa miradi ya sanaa, kama ilivyo kwa tasnia nyingine, imekua ikikumbwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa rasilimali fedha, na uwezo wa kitaalamu kutekeleza miradi yenye dhima mbalimbali.
Kuona hili taasisi isiyo ya kiserikali ilioyojikita kwenye kusaidia wasanii kwa namna tofauti tofauti, iliandaa mradi wa mfuko wa uwezeshaji ki fedha “FEEL FREE”. lLengo la mradi huu likiwa kuwawezesha wasanii kutekeleza Mawazo yao kwa uhuru kwa maana ya kwamba hamna dhima yoyote inayomlazimu msanii kuifata. Kupitia mradi huu kwa awamu nyingine tena mwaka huu 2024, wasaniii nane (binafsi na vikundi) wanaenda kunufaika kwa kupatiwa ruzuku, mafunzo na usimamizi utakaowawezesha kutekeleza miradi yao kiusanifu.
Mkurugenzi wa bodi ya Nafasi Arts Space amedhihirisha kua maombi zaidi ya 100 yalipokelewa, na baada ya mchakato, wasanii nane waliibuka videdea kupata nafasi hii kwa mwaka huu, hivyo amewasisitiza wanufaika hao kuhakikisha fedha hizo zitatumiwa kwa malengo kusudiwa.
Akizungumza na waandishi wa Habari, katika ofisi za Nafasi Arts Space, Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji na Maendeleo ya Sanaa (BASATA), Edward Buganga, ametoa pongezi kwa taasisi ya Nafasi Arts Space kwa kutekeleza mradi huu.
Vikundi na wasanii wanufaika wa mradi wa FEEL FREE ni :
Kijiweni Production (Mradi wao unaitwa Mobile Cinema yaani Sinema inayotembea, lengo ikiwa kuonyesha hadithi halisi za kienyeji na kutetea jamii zilizotengwa)
Asedeva,(Shirika lisilo la kiserikali lenye lengo la kujenga uwezo wa jamii ili waweze kushiriki kutatua changamoto zao za kijamii kupitia sekta ya ubunifu)
Ally Baharoon,((Msanii kutoka Zanzibar, mradi wake ukifahamika kama “Hadithi Hai, wenye kuleta kazi za fasihi za kienyeji kwenye uhai kupitia maonyesho ya hadhara ya jukwaani, yanayohamasisha kuthamini hadithiza nyumbani na kujivunia tamaduni zetu)
Dibembo, (msanii anaefanya sanaa ya tattoo akirudisha nyuma kwenye asili ya kabilla la Wamakonde)
Lilian Munuo,( Msanii wa sanaa za uoni na mwanaharakati wa haki za watu wenye ulemavu kutoka Kilimanjaro kupitia sanaa)
Thobias Minzi(Msanii wa sanaa za uoni, mradi wake ukiitwa SAWA, wenye lengo la kuwezesha wasanii wachoraji wa kike mkoani Mwanza ili kuficha pengo lililopo la utekelezaji wa sanaa kwa wanawake hasa wa mikoa nje ya Dar es salaam kwa kutoa elimu wezeshi kwa watakaonufaika)
Bwagamoyo Africulture (kituo cha sanaa kilichopo Bagamoyo kina lengo wakutumia tamthilia na sanaa kuchochea mabadiliko kwenye jamii)
Ikenda Tz (Mradi wao ukiitwa Batiki Mtaani, lengo wa kutoa elimu ya kutengeneza sanaa ya batiki kwa vijana wa kike waliohitimu elimu ya sekondari ili waweze kutumia elimu hiyo kujikimu kimaisha)
Mradi wa FEEL FREE umedhaminiwa na Balozi za Kifalme za Norway Tanzania na Ubalozi wa Uswizi nchini Tanzania na kutekelezwa na kituo cha sanaa “Nafasi Arts Space”