Meneja wa Shirika la umeme Tanesco Mkoa wa Kinondoni kusini Mhandisi Florance Mwakasege amewataka wananchi kuacha tabia ya kuunganisha vitu vingi kwenye kebo Moja kwakuwa ni hatari na inaweza kusababisha mlipuko ambao utagharimu maisha na Mali zao.
Mhandisi Mwakasege ametoa wito huo katika bonanza lililokutanisha wafanyakazi wa shirika hilo mkoa wa Kinondoni kusini lenye lengo la kufanya mazoezi na kujiweka fiti katika utekelezaji wa majukumu yao lakini pia kukumbushana umuhimu wa usalama mahala pa kazi ili kuhakikisha wanatoa huduma Bora Kwa wananchi.
Kupitia bonanza hilo lililofanyika katika viwanja vya Shule ya sheria jijini Dar es salaam amewataka wananchi mkoani humo kutumia wataalam wa umeme waliosajaliwa pindi wanapotaka kutandaza nyaya kwenye nyumba zao au kufanya marekebisho yeyote yale, badala ya kutumia vishoka jambo linaloweza kusababisha hatari ya mlipuko.
Bonanza Hilo limebebwa na kauli mbiu isemayo usalama kwanza likiwa na madhumuni ya kusisitiza usalama kwanza mahala pa kazi pindi wanapo kuwa wanatoa huduma Kwa wateja.