Shirikisho la soka barani Afrika CAF limetoa shukrani zake za dhati kwa Mfalme wa Morocco,Mfalme Mohamed wa Sita pamoja na mamlaka yote ya soka nchini Morocco chini ya Rais wa FA ya huko Fouzi Lekjaa kwa jinsi taifa hilo lilivokuwa na mchango mkubwa kwenye shughuli za soka barani Afrika.
Rais wa FA ya Morocco Bwana Lekjaa amesema ni matumaini ya kila mtu kuwa AFCON 2025 ijayo itakua bora kuliko zote na Morocco itahakikisha AFCON 2025 inachezwa kwa maandalizi ya kipekee.
Morocco itaandaa AFCON 2025 ambayo hivi karibuni tarehe zake zilithibitishwa ambapo mashindano haya yatachezwa Desemba 21 mwakani (2025) mpaka Januari 18 mwaka 2026.
Morocco pia itaandaa fainali za Kombe la Dunia kwa vilabu pamoja na mashindano ya Wc kwa upande wa wanawake.