Serikali imesema imeridhia mikataba mbalimbali ya kimataifa ambayo inatoa nafasi kubwa ya kuwalinda wavuvi wakiwa kazini sambamba na kuwataka wavuvi kuzingatia zaidi taarifa za mabadiliko ya hali ya hewa zinazotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini TMA lengo ni kuondoa changamoto zinazoweza kujitokeza kazini.
Hayo yamebainishwa leo na Mkurugenzi Msaidizi wa Usalama na Mazingira Wizara ya Uchukuzi Elizabeth Massawe wakati wa zoezi la usafi pembezoni mwa fukwe ya Kaole na Dunda Wilayani Bagamoyo ambapo kulikuwa na utoaji wa elimu kwa wavuvi iliyoandaliwa na Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania TASAC.
Mkurugenzi Msaidizi wa Usalama na Mazingira Wizara ya Uchukuzi Elizabeth Massawe amewatoa hofu wavuvi juu ya namna Serikali ya inaendelea kutengeneza mazingira mazuri kwa wavuvi pamoja na kuwawezesha katika nyanja mbalimbali ambazo zitaweza kuongeza kipato cha mtu mmoja pamoja na Taifa zima.
Haya hivyo nao baadhi ya wavuvi wa Wilayani Bagamoyo mkoani Pwani wameiomba Serikali iwapatie vyombo vya uokoaji ili waweze kutumia wakati wa majanga ya kuzama wakiwa katika shughuli zao za uvuvi zinazosababishwa na boti zao kutoboka na kuchoka kabisa.
Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania TASAC likiwa katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya wiki ya mabaharia Duniani linaendelea kutoaji elimu kwa wavuvi pamoja na mabaharia wadogo juu ya nafasi zao katika jamii.