Kikosi cha Kenya kitaondoka kuelekea Haiti Juni 25 kuongoza ujumbe wa kimataifa unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa kukabiliana na ghasia za magenge katika nchi hiyo ya Caribbean, vyanzo vya serikali na polisi viliiambia AFP Jumapili.
“Maandalizi yamepangwa kwa timu hiyo kuondoka kuelekea Haiti siku ya Jumanne,” afisa mkuu wa polisi alisema kwa sharti la kutotajwa jina.
Chanzo cha pili cha wizara ya mambo ya ndani kilithibitisha tarehe ya kuondoka.
Kenya imetoa maafisa 1,000 wa polisi kwa misheni ya kimataifa ya usalama nchini Haiti.
Taifa hilo la Caribbean limekumbwa na ghasia za magenge, hasa katika mji mkuu Port-au-Prince ambako maeneo makubwa yanadhibitiwa na magenge.