Israel inajiandaa kubadili hali kwenye mpaka wake na Lebanon lakini inatumai hakutakuwa na haja ya kufanya hivyo, Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu amesema, akizungumzia makabiliano yanayoendelea ya jeshi na kundi la Hezbollah la Lebanon.
Akizungumza na Idhaa ya 14 ya Israel kuhusu uwezekano wa vita kamili na Hezbollah, Netanyahu alisema ikibidi, “tutakabiliana na changamoto hii pia.
Tunaweza kupigana katika nyanja kadhaa.
Tumejitayarisha kwa hili.”
Kuhusiana na vita vya Gaza, alisema awamu ya mapigano makali inakaribia mwisho, lakini vita havitaisha hadi pale Hamas watakapoacha kudhibiti tena eneo hilo.