Wakati Vita vya Israel dhidi ya Gaza, vikiingia katika siku yake ya 263 sasa, vimewaua takribani Wapalestina wasiopungua 37,598 – wengi wao wakiwa wanawake na watoto – na kujeruhi 86,032, huku zaidi ya 9,500 wakitekwa nyara Israeli inadaiwa kujiaandaa kuanza tena kwa vita vya pande nyingi kwa mujibu wa vyombo via havari vyakimataifa.
Katika mahojiano yake ya kwanza na vyombo vya habari vya Israel tangu kuanza kwa vita, Netanyahu alizungumza kuhusu kupeleka wanajeshi zaidi kwenye mpaka wa kaskazini, na Lebanon, na kuzungumzia maandamano yanayoendelea dhidi ya serikali.
Kuhusiana na vita vya Gaza, alisema awamu ya mapigano makali inakaribia mwisho, lakini vita havitaisha hadi pale Hamas watakapoacha kudhibiti tena eneo hilo.
Netanyahu pia aliiambia Channel 14 kwamba yuko tayari kwa makubaliano “ya sehemu” ambayo yatawezesha kurejea kwa baadhi ya mateka ambao bado wanazuiliwa huko Gaza, hata kama sio wote.
“Lengo ni kuwarudisha waliotekwa nyara na kung’oa utawala wa Hamas huko Gaza,” alisema katika mahojiano na chombo cha habari cha Israel Channel 14 siku ya Jumapili.
Makumi ya maelfu ya Waisraeli wamekuwa wakiandamana dhidi ya Netanyahu na serikali yake, wakitaka uchaguzi wa mapema na makubaliano ya kuwarudisha mateka.
Mwezi uliopita, Rais wa Marekani Joe Biden alitangaza pendekezo la kusitishwa kwa mapigano, ambayo yatapelekea kusitishwa kwa mapigano kwa muda wa wiki sita pamoja na kuachiliwa kwa baadhi ya mateka wa Israel huko Gaza na wafungwa wa Kipalestina wanaoshikiliwa katika jela za Israel. Mabadilishano haya yatawezesha mazungumzo ya kusitisha mapigano ya kudumu.