Mamlaka ya usimamizi wa Bima nchini TIRA imesema inalenga kutumia maonesho ya kimataifa ya 48 ya sababa kuongeza elimu ya Bima kwa Tanzania kutoka asilimia 25 ya sasa
Akizungumza wakati akifungua kijiji cha bima kinacholeta pamoja kampuni zote 40 za huduma ya bima nchini , Kaimu kamishna bima kutoka TIRA Zacharia Muyengi amesema mpango wa serikali ni kuhakisha asilimia 80 ya watanzania wanapata elimu ya bima ifikapo mwaka 2030
Akizungumza Muyengi amesema , serikali inalengo la kuhakikisha kila mtanzania anafikiwa na huduma za bima ili kumuwezesha kujikinga na majanga
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Muungano wa Makampuni ya bima amesema sabsab ni jukwaa muhimu la kufikia wadau wengi kuwapa elimu ya bima akisisitiza wafanyabiashara kuwa na bima ili kulinda biashara inapotekea majanga
Zaidi ya kampuni arobaini za utoaji wa huduma za bima zimepiga kambi katika viwanja vya maonesho ya kimataifa ya sabasaba ambapo huduma mbalimbali za bima ikiwemo elimu ya faida za faida za bima zitatolewa kwa pamoja.