Tathmini zilizofanywa na Mfuko wa maendeleo ya Jamii ( TASAF ) zimeonyesha kuwa kaya 394,000 zainaweza kujimudu kiuchumi hivyo kuondolewa kwenye mpango wa kusaidiwa na mfuko huo huku kaya 900,000 za nchi nzima zikiendelea kubaki kwenye mpango huo.
Akizungumza hii leo kwenye ziara ya wadau wa maendeleo walio watembelea baadhi ya wanufaika wa Mfuko wa Tasaf Wilayani Kilolo Mkoani Iringa kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tasaf , Shadrack Mziray amesema mwishobwa mwezi June ,2024 utakuwa ndio mwisho mwa jaya hizo kupokea fedha kutoka Tasaf na kuanza kujitegemea wenyewe
“ wakati wa utekelezaji wa miradi hii tunafanya tathimini wale ambao Tunaona wameboreka kimaisha basi huwa wanaondolewa kwenye mpango ili kupisha wengine , na kwasasa kuanzia malipo yajayo ya ruzuku tumeshafanya tathimini na kuziondoa kaya hizo”
Na hatahivyo hadi tukamilishe tutaondoa takriban kaya 394,000 na tutabaki na kaya 900,000 na ndizo ambazo tutaendelea nazo mpaka pale awamu hii itakapo kamilika mwezi september mwakani” Amesema Mziray
Vile vile mmoja ya wanufaika wa mradi wa Tasaf Willson Mbalinga mkazi wa kijiji cha Irindi kata ya Mahenge Wilaya ya Kilolo amesema
“ wakati Tasaf inakuja kiukweli ilinikuta na hali duni sana ya kimaisha hata Mlo mmoja Kwangu ilikuwa shida ila tangu ilipoingia sasa naishi vizuri na nakula vizuri na tiari nimeshanunua kiwanja na Nimejenga na nyumba naaamini baada ya muda mchache kidogo Tasaf wakirudi watakuja kuishangaa Irindi na mimi pia maana nitakuwa nimepiga hatua kubwa sana naishukuru tasaf “ Amesema Wilson