Maafisa wa jeshi la Myanmar wamewakamata watu 11, akiwemo afisa mkuu wa Japan, kwa kuuza mchele kwa bei ya juu kuliko viwango vilivyowekwa.
Maafisa walisema Jumatatu kwamba wafungwa hao ni pamoja na wafanyabiashara wa mchele, wasagaji na wauzaji reja reja.
Mashtaka hayo yanahusiana na uuzaji wa mchele kwa bei ya hadi asilimia 70 ya juu kuliko inavyokubalika na mamlaka huku wakipambana na kuyumba kwa uchumi kutokana na mzozo unaoendelea nchini.
Miongoni mwa wa waliokamatwa alikuwa mtendaji mkuu wa Japan, ambaye kukamatwa kwake kumesababisha msuguano na Tokyo.
Mkurugenzi wa kampuni ya maduka makubwa ya Aeon Orange, Hiroshi Kasamatsu alizuiliwa kufuatia uchunguzi kuhusu viwanda vya kusaga nafaka na maduka makubwa, timu ya habari ya mamlaka ilisema Jumapili jioni.
Ilisema kuwa Kasamatsu na raia watatu wa Myanmar walishukiwa kwa upandishaji wa bei “kwa lengo la kuleta machafuko ya kiuchumi”.