Nahodha wa Mali Hamari Traore amesimamishwa kazi kwa kuchochea “uasi” baada ya kuchapishwa kwa barua ya kukosoa shirikisho la kitaifa, afisa mmoja aliiambia AFP siku ya Jumanne.
Beki wa Real Sociedad Traore alikuwa miongoni mwa wachezaji wa kimataifa ambao walichapisha barua mwezi uliopita ya kukashifu “usimamizi mbovu” na ukosefu wa taaluma miongoni mwa viongozi katika miaka ya hivi karibuni.
Wachezaji hao walitishia kuigomea timu ya taifa iwapo shirikisho hilo litashindwa kutatua mzozo ambao, wanasema, soka la Mali linapitia.
Barua hiyo iliyoandikiwa wafuasi, ilizua taharuki nchini Mali.