Ni July 3, 2024 ambapo Bodi ya Mikopo Heslb imefanya mahojiano na Clouds Media Group kuhusu kampeni mpya ya Fichua Maalumu inayolenga kuwashirikisha wananchi kwa kutumia simu na mitandao ya kijamii, kuwafichua wadaiwa sugu wa mikopo ya elimu ya juu.
“Kampeni ya fichua imelenga kuwafichua wale wanufaika waikopo ya elimu ya juu ambao wana vipato. Tunawatafuta wale wanufaika na tunataka wananchi wawafichue wale wanufaika wa mikopo ya juu ambao wana vipato ambao wamenufaika na mikopo ya elimu ya juu lakini hawajaanza kurejesha. Na kampeni inakwenda vizuri na tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana” – Dkt Bill Kiwia- Mkurugenzi Mkuu Bodi ya Mikopo.
“Tunajaribu kuwahamasisha hawa watu waweze kulipa hizi pesa zitatusaidia kuwasomesha wengine ambao nao ni wahitaji wa Miko ya Elimu ya juu”- Dkt Bill Kiwia- Mkurugenzi Mkuu Bodi ya mikopo.