Yanga SC imetangaza rasmi kuachana na Kiungo Mshambuliaji Raia wa Ghana Augustine Okrah (30) baada ya kudumu na Yanga kwa miezi sita tu.
Okrah alijiunga na Yanga SC January 2024 wakati wa Kombe la Mapinduzi ikiwa ni mara yake ya pili kucheza Nchini baada ya 2022 kushindwa kufanya vizuri na Simba SC kiasi cha kupewa mkono wa kwaheri.