Tanzania imeendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji hivyo leo kampuni ya teknolonia kutoka nchini China Sixunited Techolojia Company inayojihusisha na uzalishaji vifaa vya teknolojia imeonesha nia ya kuwekeza na kuzindua biadhaa yake mpya kwa mara ya kwanza
Hayo yamebainishwa leo Jijini Dar es salaam,2024 na Meneja wa Masoko Ukanda wa Afrika Mashariki Sixunited kampuni inayojihusisha na uzalishaji wa bidhaa za teknolojia Theresia Mwita katika hafla ya uzinduzi wa bidhaa mpya ya kisasa ya Aser Gedget(e10) lengo la kutoa bidhaa hiyo ni kusaidia upatikanaji wa teknolojia moja kwa moja kwa gharama nafuu huku na mwananchi mwenye kipato cha chini naye anufaike.
“Tumefurahishwa na ukarimu wa serikali ya Tanzania imekuwa na ukarimu mkubwa sana imetuwekea mazingira wezeshi na hivyo Uwekezaji wetu tunaoufanya kupitia kampuni yetu inayozalisha bidhaa za kisasa za.kiteknolojia kama hii ya Acer Gadget(e10) ambayo imeongeza wigo mpana katika matumizi ya teknolojia na itasaidia sekta ya elimu ” amesema Theresia
Sambamba na hayo Theresia amebainisha kuwa bidhaa ya Acer Gadget(e10) imetengenezwa kwa teknolojia ya hali ya juu kwa kwa kuzingatia maendeleo ya kidigital kuendena na soko la Dunia na pia kampuni hiyo inazalisha bidhaa zilizobobea katika utoaji wa programu za na vifaa vya akili bandia (Intelligence) ikiwemo tablet,komyuta, softcere , min pic,Oasis,seva, IoT.
“Hadi kufikia hivi sasa kampuni yetu imeajiri wafanyakazi zaidj ya 1,100 ambao zaidi ya 60% wamebobea katika masuala ya maendeleo ya utafiti,uchumj wa viwanda, mauzo na huduma” amesema Theresia
Aidha kampuni hiyo imeanzishwa mwaka 2015 mjini Shanghai nchini China imeweza kutoa huduma za suluhisho la moja kwa moja kidigitali kwa watumiaji wa bidhaa zinazozalishwa.