Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) , limewatangazia Wateja wake kuwa kutakuwa na katizo la umeme kesho Jumatatu, July 08, 2024 na Jumanne July 09, 2024 kuanzia saa 1:00 asubuhi hadi 12:00 jioni katika baadhi ya maeneo katika Mikoa 15 sababu ikiwa ni kuzimwa kwa njia kuu ya kusafirisha umeme ya msongo wa kilovoti 220 kutoka Msamvu, Morogoro hadi Dodoma(SGR) ili Mkandarasi wa TRC kuendelea kumalizia kazi zilizokua zimebaki kwenye vituo vya treni vya msongo wa kilovoti 220/27.5
Maeneo yatakayoathirika ni baadhi ya Wateja wa Mikoa ya Iringa, Njombe, Ruvuma, Mbeya, Songwe, Singida, Shinyanga, Simiyu, Tabora, Mwanza, Mara, Geita, Arusha, Kilimanjaro na Manyara.
“Kufanyika kwa zoezi hilo kutaiwezesha TRC kuweza kuimarisha mifumo ya uendeshaji treni na pia kuimarisha ufatiliaji na undeshaji wa line ya 220kv Msamvu – Dodom, Shirika linaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza”