Kiwanda Cha Sukari Mkulazi kilichopo wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro kimeanza rasmi uzalishaji wa sukari julai Mosi mwaka huu baada ya mwaka Jana kuwa katika majaribio.
Akizungunza wakati wa ziara ya Kamati ya Usalama Wilaya ya Kilosa iliyoongozwa na mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye ndio Mkuu wa Wilaya Mhe. Shaka Hamdu Shaka ,Meneja wa Kiwanda Mhandisi Aron Mwaigaga amesema tangu kuanza kwa uzalishaji huo julai Mosi tayari zaidi ya tani 300 zimezalishwa .
Mwaigaga anasema licha ya kuzliisha sukari pia wameaza kufua umeme katika kiwanda hicho ambao unatumika katika uendeshaji shughuli mbalimbali kiwandani na mwingine kuuza kwa TANESCO.
Naye Mtendaji Mkuu wa Kiwanda hicho Selestine Some amesema baada ya kuanza uzalishaji kiwanda lakini pia umeleta ajira kwa vijana wengi hasa Watanzania.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Kilosa Mhe. Shaka Hamdu Shaka amewapongeza uongozi wa Kiwanda hicho kwa hatua waliiyofikia na itasaidia kupunguza changamoto ya sukari nchini.