Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa leo ameshiriki mbio za Great Ruaha Marathon zilizofanyika ndani ya hifadhi ya Taifa ya Ruaha Ambapo lengo la kufanya mbio hizo ni kukuza utalii wa kusini na kutoa hamasa kwa jamii katika kuhifadhi mazingira
Akitoa hotuba kwa washiriki wa Mbio za Great Ruaha Marathon katika Hifadhi ya Ruaha, Mkoa wa Iringa Waziri Kassim Majaliwa Majaliwa amesema serikali ipo katika kuboresha miundombinu, ikiwemo ujenzi wa viwanja vya ndege ndani ya hifadhi na kuimarisha miundombinu yote ndani ya hifadhi
Majaliwa ameeleza kwamba mbio hizi zinaendelea kuvutia watalii kutoka sehemu mbalimbali duniani, huku zikionyesha uzuri wa uhifadhi wa maliasili katika nyanda za juu kusini huku akiwakaribisha wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuendelea kuwekeza katika maeneo ya hifadhi ikiwemo Ruaha kwani serikali inaendelea kufanya uwekezaji mkubwa ili kuvutia utalii nchini.
Hatahivyo Kuhusu barabara ya Iringa – Ruaha, ambayo imekuwa ajenda kubwa kwa viongozi wa Mkoa wa Iringa, Majaliwa alithibitisha kuwa serikali inaendelea na mipango ya ujenzi wa barabara hiyo.