Katibu tawala Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro Saidi Nguya amesema Uwepo wa huduma mbovu katika Baadhi ya ofisi za Serikali katika Halmashauri hiyo umetajwa kusababishwa na kukosekana kwa muda maalumu wa Kuwapa nafasi za kupumzika watumishi wa kada za Watunza kumbukumbu, waandishi waendesha ofisi(PS) pamoja na wahudumu
Nguya ameyasema hayo wakati akizungunza na watumishi wa kada mbalimbali kwenye Hifadhi ya Taifa Mikumi , ziara maalumu ambayo iliyoandaliwa na Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero ikiwa pia ni katika juhudi za kuunga mkono juhudi za Serikali katika kutangaza utalii wa ndani
Aidha amesema kuwa watumishi hawa wameonekana kusahaulika katika utumishi wao na kukosa muda wa kutosha wa kupumzika hivo katibu Tawala Wilaya ya Mvomero
Pia amelaani vikali kitendo Cha watumishi hawa kuonekana kudharauliwa na Sheria Kali zitachukuliwa kwa wale wote wataenda kinyume na kuwafanya watumishi hawa kukosa amani katika sehemu zao za kazi
Kwa upande wake David Kadomo kaimu mkuu wa hifadhi ya Taifa ya Mikumi ameridhishwa na kitendo kilichofanywa na Wilaya ya Mvomero hivyo ameziomba Halmashauri na Wilaya zingne kuiga mfano huu kwani kunawapa faida watumishi hawa na kuonekana wanakumbukwa muda wote.
Nao baadhi ya watumishi waliohudhuria katika ziara hii wamempongea katibu tawala kwa uamuzi mzuri alioufanya juu Yao na imewapa nguvu ya kufanya kazi kwani Jambo hili halijawahi kufanyika sehemu yoyote ile
Zaidi ya wafanyakazi 100 wa wilaya ya Mvomero wakiongozwa na Katibu tawala.wilaya hiyo Saidi Nguya wametembelea hifadhi hiyo ya Taifa Mikumi lengo ni kiendelea kutangaza vitutio vilivyopo kwenyw sekta ya utalii Mkoani Morogoro.