Hivi karibuni Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi mhe Dkt Hussein Ali mwinyi amekutana na makamu wa Rais wa benki ya uwekezaji ya umoja wa Ulaya Thomas Ostros na ujumbe wake wenye lengo la kusaidia sekta ya uchumi wa buluu hususani visiwani Zanzibar
Benki ya Uwekezaji ya Ulaya imetenga fedha za mikopo EUR 350, takriban TZS 1 trilioni Fedha hizo zimetoka kwa awamu tofauti kwanzia mwaka jana, Tanzania ilikua mnufaika mkubwa wa fedha za ruzuku kutoka Benki ya Uwekezaji ya Ulaya kutoka nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara, ambapo TSh. 758 bilioni (EUR 270 milioni) zilitengwa katika uwekezaji mpya kusaidia biashara kupitia ushirikiano na benki za kitanzania ikiwemo NMB
utiaji saini wa fedha za ruzuku umeshuhudiwa na Naibu katibu mkuu Wizara ya Uchumi Buluu na Uvuvi Zanzibar Mohammed Kharusi ambapo wenye thamani ya TZS 43 bilioni (EUR 15 millioni) baina ya Umoja wa Ulaya na Benki ya Uwekezaji wa Ulaya kwa lengo la kuwezesha mikopo isiyokua na vikwazo kwa biashara ndogondogo.
Walengwa wakuu wa fedha hizo ni biashara zinazoongozwa na wanawake katika uchumi wa bluu visiwani Zanzibar. Aidha, fedha hizi za ruzuku zitachangia na kusaidia hatua za awali kwenye mataarisho ya biashara hizo na hatimaye uwekezaji wa kibiashara.