Wakazi takribani 9600 kutoka kata tatu za wilaya ya Iringa Kunufika na mradi wa maji wa Zaidi ya shilingi milioni 500
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mkoani Iringa (IRUWASA), Mhandisi David Pallangyo ujenzi wa mradi huo wa maji safi na salama utakuwa na tija kwa wananchi huku maeneo ambayo yatanufaika na mradi huo kuwa ni wakazi wa kata ya Kalenga, Mseke, Luhota na Kiwele.
Pallangyo alisema ujenzi wa mradi huo ni utekelezaji wa maagizo ya serikali ya kutaka kuwaondoa wananchi na adha ya maji hasa wanawake kuwatua ndoo kichwani ambao ndiyo wamekuwa wahanga wa kutmba umbali mrefu kufuat huduma hiyo
Kwa upande wake mkandarasi wa mradi huo ameiomba serikali kuwezesha utoaji wa fedha za ujenzi huo kwa wakati ili kumrahisishia utendaji wake wa kazi na kukamilisha ujenzi wa mradi kwa wakati.
Mbunge wa Jimbo la Kalenga Jackson Kiswaga na mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya maji ya bunge, ambaye pia alishuhudia utiaji wa saini alisema ujenzi wa mradi huo ni utekelezaji wa dhamira ya dhati ya serikali ya awamu ya sita chini ya rais Samia Suluhu Hassan ya kutaka kumtua mama ndoo kichwani.
Kiswaga alimpongeza, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mkoani Iringa (IRUWASA), Mhandisi David Pallangyo kwa utendaji wake bora wa kazi hadi kupelekea mamlaka hiyo kuongeza maeneo ya kiutendaji ikiwemo jimboni kwake.
Kwa upande wa changamoto ya malipo ya fedha za miradi kwa wakandarasi hapa nchini, mbunge huyo amesema bado serikali inaendelea kuangalia namna bora ya kuwalipa ili miradi yote ya serikali iendele
kutekelezwa kwa wakati.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Iringa Steven Muhapa ameelezea furaha yake juu ya mradi huo, pamoja na kumuahidi mbunge huyo, usimamizi mzuri wa miradi yote ambayo serikali inatoa fedha kwaaajili ya maendeleo ya wananchi.
Nao madiwani wa kata ya Kalenga, Shakila Kiwanga na mwenzake wamemshukuru mbunge wa jimbo la kalenga pamoja na mhandisi wa mamlaka ya maji (Iruwasa) mkoa wa Iringa kwa kusimamia zoezi hilo huku wakibainisha changamoto hiyo kuwa kero kwa wananchi wa kata zao .