Kulinga na ofisi yake rais Joseph Bokai ilisema ana matumaini ya kuweka mfano wa “utawala unaowajibika” na kuonyesha “mshikamano” na Waliberia na kusema kuwa atapunguza mshahara wake kwa 40%.
Mishahara ya serikali imekuwa ikichunguzwa vikali hivi karibuni huku Waliberia wakilalamikia kupanda kwa gharama ya maisha. Takriban mtu mmoja kati ya watano anaishi kwa chini ya $2 (£1.70) kwa siku katika jimbo hilo la Afrika Magharibi.
Boakai alifichua mwezi Februari kuwa mshahara wake wa mwaka ulikuwa $13,400 na upungufu huo utapunguza hadi $8,000.
Hatua ya rais Boakai inafuatia ile ya mtangulizi wake, George Weah, ambaye alikatwa asilimia 25 ya mshahara wake.
Baadhi ya watu katika taifa hilo la Afrika Magharibi wamepongeza uamuzi wa Bw Boakai, lakini wengine wanashangaa iwapo kweli ni kujitolea kutokana na kwamba bado anapokea marupurupu kama vile posho ya kila siku na bima ya matibabu.
Kulingana na taarifa bajeti ya ofisi ya rais ni karibu $3m mwaka huu.