Waziri Mkuu wa India Narendra Modi aliwasili nchini Urusi Jumatatu kwa ziara yake ya kwanza nchini humo tangu Moscow ilipoanza uvamizi wake kamili wa Ukraine, ishara kwamba mataifa hayo mawili yanasalia karibu licha ya utegemezi wa Kremlin kwa China.
Katika ziara yake ya siku mbili, Modi alitarajiwa kuhudhuria chakula cha jioni cha faragha kilichoandaliwa na Vladimir Putin na kufanya mazungumzo na rais wa Urusi, kulingana na msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya India Randhir Jaiswal.
Lakini mkutano huo uligeuka kuwa wakukatisha tamaa baada ya kukatizwa na milipuko mapema asubuhi .
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky Jumatatu aliikosoa ziara ya mwenzake wa India huko Moscow kama “tamaa kubwa na pigo kubwa kwa juhudi za amani,” siku hiyo hiyo ambayo kombora la Urusi lilipiga hospitali ya watoto huko Kyiv.
Waziri Mkuu wa India Narendra Modi alikutana na Rais wa Urusi Vladimir Putin katika makazi yake huko Novo-Ogaryovo nje ya Moscow siku ya Jumatatu, huku umbali wa kilomita 900 (maili 560) makombora ya Urusi yakirusha miji ya Ukraine katika shambulio la mwendo wa saa moja asubuhi na kuua takriban watu 38 na kujeruhi wengine 190.