Kwenye ulimwengu wa soka leo tunamtazamia mchezaji wa zamani wa Liverpool Roberto Firmino pamoja na mkewe Larissa wame ushangaza uma baada ya kuanzisha kanisa la kiinjilisti nchini Brazil.
Roberto Firmino, nyota wa zamani wa Liverpool na Brazil, ametangaza nafasi yake mpya kama mchungaji wa kanisa hilo la kiinjilisti baada ya uwekaji wakfu ulifanyika Jumapili iliyopita, Juni 30,2024.
Katika chapisho la pamoja kwenye Instagram,mchezaji huyo wa umri wa miaka 32 na mkewe Larissa walielezea hafla hiyo kama “ya kukumbukwa na isiyoweza kusahaulika”.
Pia waliongeza:
“Kutokana na kukutana kwetu na Kristo, hamu inawaka mioyoni mwetu: ili watu wajue upendo huu ambao umetufikia. Sasa tuna shauku na wajibu mwingine: kuwa wachungaji wanaoupendeza moyo wa Mungu na wanaoshirikiana na Ufalme.”
Mabadiliko haya yanafuatia ubatizo wa Firmino mwaka wa 2020, uliofanyika kwenye bwawa la kuogelea la nyumba ya mchezaji mwenzake wa zamani Alisson.
Firmino anayejulikana kwa imani yake, mara kwa mara amekuwa akishiriki ujumbe wa kidini na picha zake akihubiri kwenye mitandao ya kijamii.
Staa huyo alijiunga na Al-Ahli ya Saudi Pro League mnamo 2023 na tangu wakati huo amecheza mechi 34 na kufunga mabao tisa.
Firmino anakumbukwa sana kwa kipindi chake cha miaka minane akiwa Liverpool, ambapo aliunda safu ya ushambuliaji ya kutisha akiwa na Mohamed Salah na Sadio Mane. Wakati akiwa na Reds, alishinda Ligi Kuu, Kombe la FA, Kombe la EFL, na Ligi ya Mabingwa ya 2021-22.
Katika hatua ya kimataifa, Firmino aliichezea Brazil mechi 55 na anashikilia rekodi ya kuwa Mbrazil aliyefunga mabao mengi zaidi katika historia ya Ligi Kuu akiwa amefunga mabao 82.
Firmino alichezea wekundu wa Anfield kwa miaka minane na kuunda safu ya ushambuliaji ya ajabu akiwa na Mohamed Salah na Sadio Mane.