Mkuu wa wilaya ya Kilosa Shaka Hamdu Shaka amefika katika Kijiji Cha Kitete baada ya kupata malalamiko kutoka kwa wananchi baada ya kukoseka huduma ya umeme katika eneo hilo licha ya nguzo za umeme kupitia ndani ya Kijiji hicho.
Wananchi hao wakizungunza wakati wa Mkutanano wa hadhara katika Kijiji hicho ambapo wamesema kuwa kumekua na propaganda kutoka kwa viongozi wao wa vijiji na kata kuwa wananchi hao wamekataa huduma hiyo Kwani kuna wachawi wengi hawataki kuonekana Kwenye mwaga.
Juma mabula Mmoja katika ya mwananchi aliyepata fursa katika makutano ambapo ameeleza kuwa wapo baadhi ya viongozi wa kata wanapeleka taarifa za uongo ngazi ya wilaya na kwamba huduma hiyo haitakiwi kijiji hapo jambo ambalo sio kweli
” mhe. mkuu wa wilaya kama tungekua hatutaki umeme umati wote huu usingekuja hapa kukusikiliza viongozi wa kata waongo Sanaa wanapeleka maneno Wilayani kuwa sisi tumekataa umeme katika Kijiji chetu tunaogopa kuonekana Kwenye mwaga”
Baada ya kupata malalamiko hayo Dc shaka akawatoa hofu wananchi kuwa serikali itahakikisha huduma hiyo muhimu anafikishwa katika vijiji vyote 138, ambapo zaidi ya vijiji 80 tayari umeme na unawaka, vitongoji 811 hatua ya usambazaji nako imeanza na inakwenda vizuri pamoja na changamoto wakandarasi kutofanya kazi hiyo kwa kasi iliyotarajiwa.
“kazi kubwa ya kuleta maendeleo inayofanywa na serikali ya Dkt Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha watanzania wote wanafikishiwa huduma hizi bila ubaguzi au dhana ambazo zinafifisha na kurudisha nyuma jitihada za mapambano ya kupunguza umasikini, ukifika umeme hapa uwekezaji wenye uhakika utafanyika, huduma za kijamii zitashamiri na mzunguko wa fedha utaongezeka kwa mtu mmoja mmoja na familia kwa ujumla”
“Wote tunafahamu umuhimu wa nishati ya umeme katika kuchochea maendeleo. Niwahakikishie Septemba 30, mwaka huu tutazindua huduma ya umeme Kitete hatuhitaji maneno mengi bali ni vitendo zaidi” alisistiza Shaka.