Kylian Mbappe amekiri kwamba mipango yake ya kuisaidia klabu yake kuchukua ubingwa wa Uropa haukufaulu baada ya Ufaransa kutolewa na Uhispania 2-1 katika nusu fainali.
Mbappe, ambaye hivi karibuni atajiunga na klabu mpya ya Real Madrid baada ya nchi yake kutolewa, alifunga bao moja pekee kwenye michuano ya mwaka huu – penalti katika sare ya 1-1 ya Ufaransa na Poland katika hatua ya makundi.
“Kwenye soka wewe ni mzuri au sio mzuri. Sikuwa mzuri,” Mbappe aliwaambia wanahabari baada ya mechi.
“Nilishindwa. Nilitaka kuwa bingwa wa Uropa… sasa nitaenda likizo, nitapumzika vizuri, itanisaidia sana, kisha nitajitayarisha kuanza maisha mapya. Kuna mengi ya kufanya.”
Mbappe aliyeangazia mashindano ya kimataifa katika miaka ya hivi karibuni hakuonekana popote msimu huu wa joto.
Mustakabali wa kocha mkuu Didier Deschamps, ambaye amekiongoza kikosi hicho kwa miaka 12, sasa unatia shaka sasa.
.