Benfica imekataa ofa kutoka kwa Paris Saint-Germain na Manchester United kumsajili kiungo wa kati Joao Neves, A Bola inaripoti.
PSG imeripotiwa kuwa na ofa ya Euro milioni 70 kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno iliyokataliwa; United pia iliona ofa yao ya €60m ikikataliwa.
Benfica itamruhusu Neves, 19, kuondoka tu katika klabu msimu huu wa joto iwapo kitita chake cha Euro milioni 120 kitafikiwa, lakini wanatumai kumbakisha kwa angalau msimu mwingine. Klabu hiyo yenye maskani yake Lisbon mwezi uliopita ilimpa kiungo huyo kuongeza mkataba, ambao ulijumuisha nyongeza ya mshahara, lakini wakala wa mchezaji huyo alikataa.
Manchester City, Liverpool na Bayern Munich pia wanavutiwa na Neves na wanafuatilia kwa karibu hali hiyo.