Japan inaonekana kuchukulia jambo la kucheka kwa uzito mkubwa na hivi sasa wameamua kujikita katika vitabu vyake vya sheria.
Kwa mujibu wa sheria, wananchi sasa wanatakiwa kucheka angalau mara moja kwa siku kulingana na ushahidi kwamba inapunguza hatari ya mshtuko wa moyo.
Sheria hiyo inatokana na karatasi ya kisayansi iliyochapishwa miaka mitano iliyopita katika Jarida la Epidemiology ambapo timu kutoka Shule ya Tiba ya Chuo Kikuu cha Yamagata ilifanya utafiti huo ambao unasema kuwa kuna ushahidi wa kutosha kwamba kicheko huja na faida nyingi kwa mwanadamu.
Sheria ya kucheka inasema kwamba raia wa Yamagata “wataongeza uelewa wao wa athari za kiafya za kicheko na kufanya juhudi kuunda afya ya akili na mwili kupitia njia kama vile kucheka mara moja kwa siku”.