Mbio za Mwenge wa Uhuru 2024 katika Wilaya ya Iramba umepitia miradi mbalimbali ya maendeleo hakuna mradi uliokataliwa.
Mbio za Mwenge wa Uhuru 2024 Wilaya ya Iramba Julai 9,2024 umekimbizwa umbali wa KM 68.1 umetembelea, umekagua, umeweka jiwe la msingi, pamoja na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo yenye thamani ya Tsh. Bilioni 5.084
Sanjari na hilo Mwenge wa Uhuru 2024 katika Wilaya hiyo umeendelea kuhamasisha na kutoa elimu kwa wananchi kupitia Ujumbe wa mbio hizo mwaka huu unaosema “Uhifadhi wa Mazingira na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa pia Ujumbe wa kudumu wa Mbio za Mwenge Uhuru katika mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI, Malaria, Dawa za Kulevya na Rushwa
Aidha miradi iliyopitiwa na Mbio za Mwenge wa Uhuru 2024 katika Wilaya ya Iramba ni mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Old Kiomboi km 1.5, Uwekaji jiwe la Msingi Shule Mpya ya Sekondari Iramba , Kutembelea mradi wa ujenzi wa chuo cha Veta ,Uzinduzi wa huduma katika jengo la Mama na Mtoto,Jengo la kujifadhia Maiti, na mitambo ya kuzalisha hewa ya Oksijeni katika Hospitali ya Wilaya ya Iramba iliyopo Old Kiomboi, Kikundi cha vijana Emirates,Kuweka jiwe la Msingi uendelevu wa Mradi wa Maji kijiji cha Makunda.
Mwenge wa Uhuru 2024 katika Wilaya ya Iramba umekimbizwa takribani kilometa 68.1 ambapo Mbio hizo zimehitimishwa leo Julai 10,2024 kwa kukabidhiwa Wilaya ya Mkalama na Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida Suleiman Mwenda, Mwenge wa Uhuru 2024 ukiongozwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndg Godfrey Eliakimu Mnzava amewapongeza kwa miradi yote kupita kwa kishindo.