Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) limesema jumla ya wombaji 16,646 wamechaguliwa kujiunga kwenye vyuo 221 vinavyotoa programu mbalimbali za Afya na Sayansi Shirikishi.
Akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Twaha Twaha MENEJA was Kitengo cha Utunuku na Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Udahili, Utahini na Utunuku Dr.Marcelina Alloyce amesema katika idadi ya waliochaguliwa wanawake ni 8,821 (53%) na wanaume ni 7,825(47%).
“Jumla ya waombaji 24,629 waliwasilisha maombi yao kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS). Waombaji 23,503 walikamilisha maombi yao kwa kuchagua vyuo/programu walizozipenda,”
“Pia waombaji 21,661 walikuwa na sifa kwenye programu walizoomba na waombaji 1,842 hawakuwa na sifa kwenye programu walizoomba,”.
Aidha, waombaji wenye sifa ambao hawakuchaguliwa kutokana na ushindani katika
programu na vyuo walivyoomba wanashauriwa kuomba kujiunga katika programu na vyuo vyenye nafasi katika dirisha la awamu ya pili kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja.